Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira (wa pili kulia), Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli(kulia),Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SSP Pili Misugwa (kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Liston Matacha na Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt, David Tarimo wakifurahia kwa kupiga makofi baada ya uzinduzi rasmi wa mbio za Kilimanjaro Marathon uliofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon uliofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, Mkoani Kilimanjaro.