Na Collin Ndanzi, Globu ya Jamii,


Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameutaka uongozi wa klabu hiyo uweze kumsajili Edinson Cavani baada ya mchezaji huyo kuwasilisha maombi ya uhamisho klabuni hapo. 

Edinso Cavani amekuwa si mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu klabu ya PSG kumsajili Mauricio Icardi kwa mkopo akitokea Inter Milan ambae amekuwa chagua la kwanza la kocha wa klabu hiyo Thomas Tuchel.


Cavani (32) ambae alijiunga katika klabu ya na klabu ya PSG 2013, ameweza kushinda magoli 198 katika mechi 292 ambazo ameitumikia klabu hiyo. Lakini mchezaji huyo anaonekana kutaka kikwazo kingine nje ya PSG ma mashabiki wa Manchester United wanaona kama ni mbadala wao.


Kwa sasa timu  ya Manchester United ipo katika kipindi kigumu baada ya nyota wao tegemezi kuwa majeruhi wakiwamo mshambuliaji Marcus Rashford, na viungo Paul Pogba na Scott Mctominay ambao pia wapo majeruhi.


Kwa sasa klabu ya Manchester United wako kwenye utegemezi wa Mason Greenwood, Daniel James na Antony Martial ambae anatokea majeruhi. 

Hivyo mashabiki wa Manchester United wanaona kama ni wakati sahihi wa klabu hiyo kumsajili Cavani ambae ataongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.


Klabu kadhaa zimekuwa zikiwania saini yake ambapo Atletico Madrid na Tottenham wanaonekana kuwania saini ya mchezaji huyo, lakini mashabiki wa klabu ya Manchester United wanaona Cavani kama ni mchezaji ambae atakuwa msaada mkubwa wa klabu hiyo.


Mwenyekiti wa klabu ya PSG, Leonard amesema kuwa klabu imeshapata ofa kutoka kwa Atletico Madrid, lakini kiwango cha ofa hiyo bado hakijawaridhisha kutokana na thamani ya kiwango cha mchezaji huyo raia wa Uruguay kutolingana na ofa iliyotolewa, hivyo wanasubiri ofa ambayo inaweza kuwashawishi kumuachia mchezaji huyo.


Manchester United ambayo imetoka kupoteza mchezo dhidi ya Liverpool ambapo wanaonekana kutokuwa vizuri katika eneo la kushambulia hivyo mashabiki wa klabu hiyo wametoa mapendekezo kadhaa juu ya usajili wa mchezaji huyo.