Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Mhandisi Kadaya Balyhye akitoa maelezo kuhusiana utaratibu wa leseni kwa mafundi zinazotolewa na mamlaka hiyo. 
 Mkuu wa Kanda ya mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na mafundi simu mkoa Morogoro kuhusina na umuhimu wa mafundi simu kuwa leseni.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba akitoa maelezo kuhusiana na mafundi siku kuwa leseni katika mkutano. 
Baadhi ya mafundi Simu wa mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa na Watendaji wa TCRA na Manispaa Morogoro. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa Mafundi simu wote wanatakiwa kuwa leseni kutoka mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na weledi wa kazi wanazozifanya. 

Akizungumza na mafundi simu wa Manispaa ya Morogoro Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania , Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa mafundi simu ni kazi nyeti hivyo lazima wawe na leseni kazi hiyo na kuendelea kutengeneza simu bila leseni ni kosa la jinai. 

Amesema kuwa mafundi simu hao wanatakiwa kupata leseni ikiwa ni kupatiwa mafunzo kwa TCRA kushirikiana na wadau ambao na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam. 

Odiero amesema mafundi simu wakiwa na mafunzo watakuwa ni watu kulinda usalama wa mawasiliano ikiwa ni kuweka utaratibu wa kuwa na vitabu vya kusajili simu na kuuliza simu historia ya kabla ya kutengeneza kwa wateja wao simu walikozitoa ili kuondoa wizi wa simu. 

“Hakuna sababu ya fundi simu kutengeneza simu ambayo mwisho wa siku taarifa za simu hazieleweki ndipo hapo mtu anaingia katika tatizo lisilomhusu lililotokana na kushindwa kuwa kutokuwa na taarifa za simu ya mteja”amesema Mhandisi Odiero. 

Aidha amesema kuwa kwa mafundi simu kuwa na umoja kutarahisisha TCRA kufanya mawasiliano kwa mafunzo ambayo yatakuwa yameandaliwa ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kuzingatia matumizi ya simu kutoka kwa wateja. 

Nae Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Ipyana Haraba amesema kuwa mafundi simu ni watenda kazi hivyo ushirikiano unahitajika kutambua wanaofanya nje ya utaratibu na sheria itashika mkondo wake. 

Mhandisi Baluhye amesema kuwa mafundi simu nchini wakisajiliwa ni fursa ambapo serikali iko katika uchumi wa viwanda hivyo kunaweza kutokea kiwanda cha simu au kuunganisha simu mafundi wataotumika ni wa ndani. 

Mwenyekiti wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba amesema wameweka mkakati wa wa mafundi simu wote wawe wamejisajili katika umoja huu kurahisisha utoaji huduma na mafunzo ya weledi yatakyotolewa na TCRA. 


Haraba amesema kuwa safari imeanza kwa mafundi simu kuweka utaratibu wa mazingira ya kufanya kazi na vyombo vingine ikiwemo jeshi la polisi kushiriana katika kubaini wezi wa simu.