Mamlaka ya Liberia imesema kwamba inarejesha shehena nne nchini Ugiriki zilizojaa tani za mifuko ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira

Mifuko hiyo ilikuwa imeingizwa nchini humo kimagendo kwa kisingizio kwamba inaweza kuchakatwa upya lakini Maafisa wa Kupambana na Bidhaa za Magendo waliibua malalamishi katika Bandari ya Monrovia pale mzigo ulipowasili ukiwa unanuka uvundo na kutoa harafu mbaya
-
Baada ya kontena hizo kukaguliwa, Shirika hilo limesema kuwa aina ya mifuko ya plastiki iliyoletwa, imepigwa marufuku kuchakatwa na kutumiwa tena nchini Ugiriki

Aidha uchunguzi umeanzishwa mara moja kuhusu namna mzigo huo ulivyoagizwa