Msanii wa filamu nchini Jacqueline Wolper, amesema siku atakayopagawa ndiyo atam post mpenzi wake pia yeye ni mmoja wa watu ambao wanalitangaza vyema Taifa kwa kuwa na mpenzi nje ya Nchi.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Jacqueline Wolper amekiri ni kweli ana mpenzi mpya nje ya nchi, huwa anawasiliana naye mara kwa mara na akimkumbuka huwa anamfuata huko alipo.

"Mnataka hadi muone tunapost wapenzi wetu ndiyo mjue kama yupo, sasa hivi nipo huru sana naona kama nimezaliwa upya yaani, nimebadilika sana ila siku nitakayopagawa nitampost bado sijapagawa na sijataka, mpenzi ni ninaye na tunawasiliana, unadhani nitakaaje sasa kwa kuwa yeye yupo mbali na hatuishi pamoja wala nchi moja" ameeleza Jacqueline Wolper.

Aidha Jacqueline Wolper ameongeza kusema "Kutoishi naye pamoja kunafanya mara chache sana kuwa kimapenzi na sasa hivi nipo kikazi zaidi, nikimkumbuka nitaenda kumfuata au yeye atakuja naitangaza vizuri sana nchi".