Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani (Kulia) akizungumza na waandishi wa haari jijini Dare es Salaam leo wakati wa kuzindua kampeni ya Usalama wa Reli kwa kuzuia ajali, uhalifu na hujuma katika Reli ya Shirika hilo, ambayo itakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa Rasilimali za shirika Reli hapa nchini. Kushoto Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi, Stanslaus Kulyamo.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani (Kulia) akizungumza na waandishi wa haari jijini Dare es Salaam leo wakati wa kuzindua kampeni ya Usalama wa Reli kwa kuzuia ajali, uhalifu na hujuma katika Reli ya Shirika hilo, ambayo itakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa Rasilimali za shirika Reli hapa nchini. Katikati Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi, Stanslaus Kulyamo.Kushoto ni Ofisa Habari wa Shirika la Reli Tanzania, Jamilla Mbarouk.
Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi, Stanslaus Kulyamo akizungumza za waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua Usalama wa reli hapa nchini.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Habari wa Shirika la Reli Tanzania, Jamilla Mbarouk akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua kampeni ya usalama wa Reli.
Na Mwandishi Wetu.
KUNA baadhi ya wananchi wasio wema wana hujumu Reli kwa kutega vyuma mawe makubwa pamoja na kuiba waaswa kuacha tabia hiyo kwani Serikali inatambua hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usalama wa Reli kwa kuzuia ajali, uhalifu na hujuma katika Reli ya Shirika ambayo itakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa Rasilimali za shirika hilo.
"Wanaohujumu miundombinu ya reli wanatakiwa kuacha mara moja ili kuepusha ajali, uharibifu wa miundo mbinu hiyo inayoweza kusababisha vifo, majeruhi na hasara itokanayo na uhujumu huo". Amesema Sahani
Hata hivyo sahani amewaomba wananchi, taasisi zisizo za kiserikali, viongozi wa serikali kutoka ngazi za vijiji, mikoa na taifa kutoa taarifa kupitia namba 0800110042 kwa yeyote anayehujumu miundombinu ya reli.
Ili kuweza kuimalisha usalama wa reli hapa nchini kila mwananchi anatakiwa kuheshimu alama zilizowekwa kwenye makutano ya barabara na reli, Kujiepusha na uharibifu wa mazingira unaopelekea miundombinu ya Reli kuharibiwa na maji ya mvua.
Hata hivyo wananchi wanataikiwa kutoa taarifa katika shirika la reli Tanzania ya viashiria vyovyote vinavyoweza kupelekea kuathiri usalama wa reli.
Kwa upande wa madereva wa magari, pikipiki na baiskeli wawe waangalifu wanapoelekea kukatisha vivuko vya Reli, wananchi wajiepushe kufanya shughuli za kijamii pembezoni wa Reli, kwenye hifadhi ya ardhi ya Reli ya mita 60, kwenye mipaka stesheni pamoja na kuharibu kingo za mito.
Licha ya hayo Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi, Stanslaus Kulyamo amewaasa wananchi wote waohujumu miundombiinu ya reli kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi kitengo cha Reli wapo katika mikoa yote ambapo Reli inapita.
Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi wote wanaopitiwa na miundo mbinu ya Reli, waone reli hiyo kama ni mali yao na ni mali ya watanzania wote na imejengwa kwa kodi ya wanchi waachane na kuhujumu miundombinu hiyo.
Hata hivyo Mkuu wa Kitengo cha sheria Shirika la Reli Tanzani, Veronika Sudai amesema adhabu itakayotolewa kwa mtu yeyote atakayeonekana kuhujumu miundo mbinu ya Reli kwa mujibu wa Sheria ya Reli ya 79 ibara ya 1 ya mwaka ya 2017.
Atakaye hujumu miundombinu hiyo atalipa faini ya shilingi milioni 50 au kifungo cha miaka mitatu jera, ama vyote kwa pamoja yaani kulipa faini ya milioni 50 na kwenda jera miaka mitatu.