Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania ambaye ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa pakubwa katika eneo la Afrika mashariki Rajab Abdul Kahali maarufu Harmonize ametoa ujumbe.

Amewataka vijana kukabiliana na changamoto wanazopitia kwa lengo la mafanikio

''Kila kitu kinachotokea katika maisha yake kichukue kama changamoto , ni muhimu kukabiliana nacho na kuthibtishia watu kwamba unaweza kupambana nacho'' , aliambia kipindi cha muziki cha BBC, Hii ni Afrika.

Kabla ya kuwa msanii maarufu nchini Tanzania , Harmonize alionekana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha kuonyesha talanta na aliambiwa na majaji kusahau kuhusu muziki.

Hatahivyo kwa bahati nzuri alipuuzilia mbali ushauri wa majaji hao wa muziki na kuendelea na kile alichoona ni kipaji.

''Nilijua kwamba nilikuwa na kipaji hivyobasi niliendelea kujifunza muziki licha ya ushauri wa majaji wale''.

Hatimaye kujiamini kwake kulizaa matunda na hii leo Harmonise anajivunia mamilioni ya wapenzi wa muziki wake katika mtandao wa You Tube.

Licha ya msanii huyo kuchukuliwa na nyota wa muziki wa bongo fleva na msanii aliyefanikiwa zaidi Afrika mashariki Diamond Platinumz kwa sasa ameamua kuchukua safari yake pekee baada ya kujiondoa katika kundi la muziki la Wasafi.