Kuna msemo wa kiswahili unasema ukifuga chatu uwe na unga wa kumlisha, kwa maana ukiishiwa unga atakugeuza wewe ndio msosi wake.
Hii ni sawa na team ya Wasafi wanavyomuendekeza Dudu Baya aka Konki masta.
Kwa sasa Dudubaya amekuwa msema hovyo kupitia page yake ya Instagram na kwa sababu anasema yanayowapendeza Wasafi basi wameamua kumuendekeza na kumpa platform ya ku-shine.
Lakini niwataadharishe tu Wasafi ipo siku Dudu Baya atawageuzia kibao sababu ukimtazama kwa makini anapozungumza na vitu anavyozungumza unaona kabisa huyu mtu ana shida kichwani. Yani kwa kifupi Dudu baya kwa sasa afya ya akili yake Ina mushkeli.
Anaweza kuwa anaongea mengi yenye ukweli lakini kusema ukweli pekee akutoshi kuonesha uzima wa akili yake, maumivu na kutotendewa haki kwenye muziki wamefanyiwa wengi sana tena waliofanya makubwa kwenye muziki lakini watu wameanguka wakasimama na maisha yanaendelea, kina P Funk Majani wamefanya kila kitu kwenye muziki lakini walilizwa na wadau ila wakachagua busara zaidi maisha yanaendelea.
Dudu baya ni mtu anayeonekana ana hasira, amechanganyikiwa na ana msongo wa mawazo asiyejua kesho yake inakuwaje.
Nawashauri Wasafi kaeni mbali na Dudu Baya, au msaidieni aende rehab akatibiwe.