Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemuandika  barua ya wito msanii wa bongo flea Godfrey Tumaini maarufu kama dudu baya kutokana video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonesha msanii huyo akitoa maneno yasiyo na maadili.

Basata imemtaka msanii huyo kufika katika makao makuu ya baraza siku ya jumanne January 7,2020 mnamo saa nne kamili asubuhi.

Katika barua hiyo Baraza limesikitishwa na kauli zisizokuwa na maadili wala staha kupitia video zilizorushwa kupitia mitandao ya kijamii zikimuonesha msanii huyo akitoa lugha zisizokuwa na maadili


Aidha wameadika kuwa Baraza la sanaa ni chombo kilichoundwa kisheria kusimamia, kukuza na  kuendeleza sekta ya sanaa hapa nchini