Imeripotiwa kuwa Mtanzania Dkt Luis Shika aliyewaho kujizolea umaarufu kote nchini kutokana na kitendo cha kutaka kununua nyumba za serikali zilizokuwa zinapinga mnanda amelazwa katika hospitali ya mwananyamala akisumbuliwa na ugonjwa usiojulikana na rafiki zake za karibu

Dkt Shika ambaye kwa sasa maisha yake inaalezwa kuwa analala kwenye kituo kimoja cha daladala jijini Dar es salaam bado haijulikani ni ugonjwa gani unaomsumbua

Mganga wa zamu wa hospitalini ya mwanayamala Bernadetha Mosha amethibitisha kumpokea Dkt Shika akitokea hospitali ya Sinza


“Tumempokea jana jioni na tulimpatia matibabu katika kitengo cha dhalula hali yake ni swali “

Ikumbukwe kuwa Dkt Shika aliwahi kusema kuwa ni tajiri anayemiliki pesa nyingi zilizopo nchini Urusi hivyo anasubiria zitume nchini ili aweze kutumia