Msanii Daimond platinum amerejea nchini na kufunguka show yake aliyoifanya katika tuzo za CAF ambazo zilifanyika nchini misri ikiwa kwake ni mara ya pili na kusema kuwa ilikuwa nzuri kwakuwa waandaaji walijipanga.
Akifanyiwa mahojiano na wasafi media amesema kuwa yeye ndo msanii pekee toka Afrika ambaye alipata nafasi za kualikwa na kufanya show katika tuzo hizo na kusema kuwa kati ya show zake zote hii ndo alilipwa vizuri.
''Kiukweli Nimefanya Show Nyingi na Malipo ya Show Hii ya CAF Nililipwa Vizuri sio Uongo na
nimehudhuria Tuzo nyingi sana Duniani, lakini tuzo za CAF Kiukweli Jamaa Walijipanga sanaaaaa kwasababu walikuwa na maandalizi ya Hali ya juu'' alisema Daimond.