Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na C.E.O wa Wasafi Media Diamond platnumz ametuma video ikionyesha anasikiliza wimbo wa msanii mwenzake ambaye Alikiba na kuamua kuipost kwenye mtandao wake wa instagram.

Diamond ambaye anajulikana kuwepo kwenye bifu kubwa na Kiba ameamua kuonyesha hisia zake kwa kusikiliza wimbo wa 'hadithi na kusema kuwa dio wimbo wake bora kutoka kwa Kiba.

Diamond alirekodi video hiyo mara tu baada ya kutua Dar Es Salaam akitokea KIGOMA baada ya kumaliza show yake ya miaka 10 akiwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.