Mgeni rasmi katika hafla fupi kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera na Wateja wa benki ya CRDB, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiwa ameongoza na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi wa hoteli ya Smart, iliyopo mjini Bukoba jana. hafla hiyo iliandalia na Benki ya CRDB kwa lengo la kupata chakula cha jioni pamoja na kubadilishana nawazo na wateja hao. Kulia Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya kukutana na baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera na wateja wa Benki ya CRDB, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Smart, mjini Bukoba. Wengine pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania, Ladislaus Matindi (wa pili kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza katika hafla hiyo, iliyowakutanisha wafanyabiasha wakubwa wa mkoa wa Kagera pamoja na wateja wa Benki ya CRDB, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Smart, mjini Bukoba. ambapo aliipongeza Benki kwa kuweza kuwafikia wateja wake wa kada zote na kuwafata popote walipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla hiyo, iliyowakutanisha wafanyabiasha wakubwa wa mkoa wa Kagera pamoja na wateja wa Benki ya CRDB, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Smart, mjini Bukoba.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora akizungumza machache katika hafla hiyo, iliyowakutanisha wafanyabiasha wakubwa wa mkoa wa Kagera pamoja na wateja wa Benki ya CRDB, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Smart, mjini Bukoba.