STAA wa Bongo Muvi; Aunt Ezekiel amesema kitendo cha shosti wake wa kitambo Wema Sepetu kurudisha urafiki wake kwa muigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ hakimsumbui chochote kwa sababu kila mtu ana maamuzi kwenye maisha yake.  Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt amesema kuwa katika maisha hakuna mtu anayelazimishwa kuwa na rafiki mmoja na yeye Wema ni binadamu kama walivyo wengine, anaweza kuchanganya marafiki.

“Yaani nashangaa sana kila mtu ananiambia na kuniuliza Wema karudiana na Batuli, sasa wakirudiana inanihusu nini jamani? Yeye ni binadamu, anapaswa kuwa na rafiki yeyote anayempenda na sio kwa ubaya,” alisema Aunt. Siku za hivi karibuni, Wema ameonekana kuwa karibu sana na Batuli huku Aunt akionekana kuwekwa pembeni kiaina.