Asiwaze Lyrics – Stamina Ft Atan – New Song

Asiwaze Lyrics – Stamina Ft Atan

Iye iye iye iye iyeee iyee
Iye iye iye iye iyeee iyee

Asiwaze Lyrics Verse One

Unaposkia neno ndoa, ujue noma
Kabla kuongea chochote,
naomba kwanza kusonya
Phhwwwwww phwwww
Sijali nishauri nani aisee ok twende

Aliyenifundisha mapenzi
Hakuniambia kuhusu kuoa
Alinionyesha staili za tendo
Ila sio maisha ya ndoa

Aliyesema ndoa ndoano
Hivi mjinga ni nani
Kafanya nivue samaki
Kwenye bahari yenye tsunami

Nikiziona picha za harusi
Najiskia vibaya
Namuonea huruma padri
Pamoja na waimba choir

Yale mafunzo ya katekista
Eti yamepotea mazima
Sadaka misa ya ndoa
Bora mngewapa watoto yatima

Pole wasimamizi wa ndoa
Kwa ujinga mliosimamia
Mngesimamia ukucha
Mngekuza hata familia

Kama ni pete, nisharudisha kwa sonara
Tayari nimeshavuta mpunga nimerudisha nusu hasara
Kabla kuingia ndoani anakuwa kondoo usiyemjua
Ila ukimweka ndani nyani anakuachia mabua

Marafiki mashemeji ndio wanafiki nakuambia
Wanaweza kufanya ulewe bila hata kukupa beer

Saasa ile suti, nilivaa ya nini     Na mchango, nilichangisha ya nini
Na wale ndugu, niliwaita wa nini   Na kile kiapo, niliapa kwa nini

Chorus

Naubembeleza upepo
Usizime kibatalii
Iye iye iye
Kichwani mwangu hayupo
Moyoni niko shwari

Wanajaa jaa pengo mwambie asiwaze
Huko aliko atulie asiwaze
Kama amepoteza lengo mwambie asiwaze
Huko aliko atulie asiwaze

Asiwaze Lyrics Verse Two

Mwambieni yule dogo aliyeichezea club ya simba
Kutembea na mke wangu asijione ameshinda mi samaki
Mapenzi yangu yana chombo kaka nishakula sio nuksa kutoa vyombo
Hata posa nililotoa mwambieni aingize vikoba

Ila atakaye muoa ampe mtaji wa bodaboda
Ama kweli hii dunia ina mambo mengi
Na ndoa ni kama boati haiwezi kuparki stendi

Hichi cheti cha ndoa nimebaki nacho kwa nini
Siwezi kuombea kazi Hakina mchongo apa mjini
Hata biblia imeandika wanawake tuishi nao kwa akili
Kwao sikumficha kitu ulimpa hadi sehemu za siri

Akiskia nimekufa mwambieni asilie sana
Aite rafiki wafurahi wachome nyama
Nitazikwa na ndugu rafiki na mafans kibao
Mkimuona msimbane nitafufuka nimzabe vibao

Unaweza kumpakia mkongo mkeo na usimfikishe
Alafu anayempakia mkorogo ndio akamfanya amridhishe
Ndoa ndoana anayebisha aniulize mimi
Nishawahi kuwa na mahusiano ambayo sijui yanahusiana na nini

Na ile keki, nilikata ya nini Na mahari, nililipa kwa nini
Na yule mchenga, nilimtuma wa nini  We Si uliyaapa tena ukala yamini

Chorus

Naubembeleza upepo
Usizime kibatalii
Iye iye iye
Kichwani mwangu hayupo
Moyoni niko shwari

Wanajaa jaa pengo mwambie asiwaze
Huko aliko atulie asiwaze
Kama amepoteza lengo mwambie asiwaze
Huko aliko atulie asiwaze

Verse Three

We ambaye hujaolewa
Usifanye kama hutaki kuolewa hivi
Alafu na we hujaoa
Sio kwa sababu ya nyimbo hii eti ukakata tamaa ya kuoa
Sijaema hivo aiseee

Asiwaze, hata akinisema popote pale Asiwaze, na hata tukionana popote pale Asiwaze, bear peace i live my life men

The post Asiwaze Lyrics – Stamina Ft Atan – New Song appeared first on cloudsmediatz.