Mtume Paul Toritseju (kushoto)  kutoka Nigeria akizungumza wakati akitoa mada katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja,  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkalimani wake,Mwenyeji wa Kongamano hilo, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick.

Mwenyeji wa Kongamano hilo, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick, akisisitiza jambo.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
Mafundisho kwa vitendo katika  Kongamano hilo. 
 Mtume Paul Toritseju (kushoto)  kutoka Nigeria, akimkabidhi kitabu, Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa.
 Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa, akionesha kitabu hicho.
 Mwamasishaji wa vijana kufikia mafanikio, Mhandisi Nicholaus Moses akizungumza katika kongamano hilo.
Mmoja wa wachungaji akitoa neno la shukurani katika kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

VIJANA wametakiwa kuwa na maono makubwa ili wainuke kiuchumi na kuwa na fedha badala ya kulalamikia kuwa maisha ni magumu.

Wito huo umetolewa na Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria wakati akitoa mada katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja,  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

" Ukitaka ufanikiwe kwanza kabisa ni lazima uwe na maono na kuyafanyia kazi na si vinginevyo" alisema Toritseju. Aidha alisema mafanikio yanaanzia kichwani, ndani ya mtu na si kwa nje au kinachoonekana

Alisema haiwezekani mtu akawa tajiri lakini hafanyi kazi hapo ni lazima watu watalazimika kuuhoji utajiri alionao.

Alisema vijana wanapaswa kubadilisha mtazamo wa akili zao ili kuyaendea mafanikio na kuwa tatizo la umaskini linaanzia rohoni kwani mtu anatakiwa kuwa na nguvu na roho mpya.

Alisema mpango wa mungu ni vijana kuimarika kiuchumi na  kuongeza idadi ya vijana wengi zaidi kimafanikio. Hakuna kijana aliyemtegemea Mungu na akawa maskini

Alisema Afrika tunafikiria zaidi watoto badala ya kuwa na mipango madhubuti ya kuanzisha biashara katika nyanja mbalimbali kama mawasiliano, utamaduni, ujenzi wa viwanja, elimu, kuanzisha blog na kuwa na mawazo mapya.

Alisema changamoto nyingine kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni matumizi ya mitaala ya elimu ya kizamani ambayo walitumia wazazi wetu iliyopitwa na wakati na sasa kuna mabadiliko makubwa na mambo mengi ni mapya.

Mwezeshaji mwingine katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa akilitoa mada kuhusu kijana kama kiongozi kwa ajili ya mafanikio ni lazima asimamie misingi iliyopo ili aweze kumiliki uchumi ambayo ni maono, malengo, kutumikia wengine, kusali, kutomdharau mtu wala kudharauliwa, kanuni za utunzaji wa fedha, kwenda na muda na kuwa na mauhusiano na watu mbalinbali.

Alitaja mambo mengine ya kuweza kumfikisha kijana katika mafanikio kuwa ni kuthubutu, jitihada na kufanya kazi kwa nguvu.

Dkt.Mbelwa alisema mafanikio hayo yatapatikana kwa kuwepo maono, kujua unapoelekea na kuwepo kwa taarifa na kama hakuna taarifa huwezi kufanya chochote.

Akizungumzia suala la viongozi alisema hawachaguliwi bali wanaandaliwa na kuwa pasipo taarifa huwezi kuwa na kiongozi hivyo alihimiza watu wasome sana vitabu ili kupata maarifa na si kupoteza muda katika mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na mingine.

Mwenyeji wa Kongamano la Kwanza la  vijana, 2019,  Mchungaji Dkt.  Sako Mayrick alizungumzia umuhimu wa vijana wa kuwa na maono kwa ajili ya kumiliki uchumi kwa kusisitiza kuwa hapa duniani hakuna bosi bali tumeumbwa kutumikia wenginena watu waache uvivu na uzembe. 

Aidha,  vijana wametakiwa kuwa na nidhamu katika maisha hususan katika matumizi ya fedha na muda. Kongamano  la pili la  Vijana litafanyika Desemba, 2020. Success Chapel ni Huduma ya kumsaidia mwanadamu afikie uwezo wa ufanisi na kupata mafanikio katika nyanja zote na fedha