Kutokana na pori la akiba la selous kugawaywa na kuwa hifadhi ya taifa ya Nyerere kamishna Mkuu wa uhifadhi TANAPA Dkt. Allan Kijazi amewaondoa shaka wawekezaji wote ambao waliingiwa na wasiwasi kuwa mgawanyo wa pori hilo utaathiri shughuli zao za uwekezaji.

Kamishna mkuu wa uhifadhi Tanzania (TANAPA) Dkt Allan Kijazi amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau wa hifadhi ya taifa ya Nyerere kilicholenga kutoa uwelewa namna hifadhi itakavyoendeshwa chini ya usimamizi wa TANAPA ambapo ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya pori hilo zipo shughuli ambazo zitasitishwa na nyingine zitaendelea kwa mjibu wa sheria za TANAPA huku mwakilishi wa kamishna wa uhifadhi mamlaka ya wanyamapori Tanzania (TAWA) Zahoro Kimwaga amesema watakakikisha nia ya pori la selous kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi inafanikiwa kwa kushirikiana na TANAPA.
Kamishna mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania TANAPA Dkt, Allan Kijazi akifungua kikao kazi cha wadau wa Utalii hifadhi ya Taifa ya Nyerere kilichofanyika katika taasisi ya utafiti wa misitu (TAFORI) Morogoro kujadili namna bora ambavyo hifadhi itaendeshwa chini ya usimamizi wa TANAPAna kuwaeleza wawekezaji kuwa mabadiliko na mgawanyo wa pori la akiba hautasababisha mtikisiko wa kibiashara.
Wadau wa utalii wakifatilia kwa umakini historia ya pori la akiba Selous hadi kugawanywa kuwa hifadhi ya taifa kikao kilichofanyika mkoani Morogoro.
Kamishna mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania TANAPA Dkt. Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na wadu wa utalii mara baaada ya kufungua kikao kushoto kwake mwenye koti ni mwakilishi wa kamishna wa uhifadhi mamlaka ya wanyama pori Tanzania (TAWA) Zahoro Kimwaga.
Meneja wa poli la akiba Selous Enock Msocha akielezea historia ya pori hilo kwa wadau wa utalii katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Morogoro.
Kamishna mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania TANAPA Dkt. Allan Kijazi na mwakilishi wa kamishna wa uhifadhi mamlaka ya wanyama poli Tanzania (TAWA) Zahoro Kimwaga wakifatilia wasilisho la historia ya pori la akiba linalotolewa na meneja wa pori la akiba Selous Enock Msocha katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Morogoro.