Msanii na mtayarishaji wa muziki, Nuh Mziwanda, amefunguka madai ya kumtenga na kutomsaidia rapa Chid Benz, ambaye ni Kaka yake wanaotokea Mtaa mmoja maeneo ya Ilala,Jijini Dar es Salaam.

Akifunguka kupitia EATV & EA Radio Digital, Nuh Mziwanda amesema hajamkataa Chid Benz, ataendelea kuwa Kaka yake, ambaye anampa ushauri hata kama hajawahi kumsaidia chochote.

"Sijamkataa Chid Benz na kwanini nimkatae yule ni Kaka yangu, namuheshimu sana mimi ni dogo kwake, wakati yeye anatoka hata kumsogelea mtaani nilikuwa nashidwa, hakuna kitu kama hicho akilini mwangu kwamba sipo tena na Chid Benz, itakuwa sio Ilala tena kwa sababu sisi wote ni watoto wa mtaa mmoja" amesema Nuh Mziwanda.

Aidha Nuh Mziwanda ameendelea kusema "Yule ni Kaka yetu bado tupo naye, mimi nakutana naye tunapiga stori na ananishauri mambo mawili matatu, sio kama tunamtenga au ametutenga kwa sababu ametuzidi yeye ni msanii mkubwa kwetu na tupo sawa" ameongeza.