Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nay wa Mitego ametumia ukurasa wake wa Instagram kutupa dongo kwa Diamond kuhusiana na tamasha la Fiesta lili;ofanyika wikiendi hii katika uwanja wa uhuru jijini Dar Es Salaam.



Ikumbuykwe baada ya Tamasha la Wasafi Festival kumaliuzika tarehe 9 mwezi wa 11 na kufanikiwa kujaza uwanja kwa asilimia kubwa ambako lilifanyikia katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaam yalianza maneno ya kukejeliana kati ya pande mbili ambazo zimefanikiwa kufanya matamasha makubwa hapa nchini ambalo ni Tamasha la Wasafi Festival lililochini ya Wasafi Media na Tamsha la Fiesta lililochini ya Clouds media.

Maneno yalianza baada ya Tamasha hilo kujaza sana na watu kuanza kusema kuwa tutaona tamasha la Fiesta kama litajaza hivi lakini pia katikati kabla ya Tamasha la Fiesta kufanyika Dar Es Salaam yaliibuka maneno baada ya Diamond kwenda kufanya show nchini Siera lione na kufanikiwa kujaza uwanja watu walianza kumkejeli kuwa haikuwa show yake, na kupelekea Diamond kuandika maneno haya:-

“Mama See how much SIERRA LEONE Loves your Son😭😭😭…. 70,000+ STADIUM #SOLDOUT Last Night!…. i can’t even Explain how Grateful i am SIERRA LEONE 🇸🇱❤🇸🇱….. GUINNÉ BISSAU we fill LINO CORREIA STADIUM this Saturday Dec 7th🙏🏼…. CAMEROON Douala National stadium Dec 20th 🛸🌍🛸Kuna Baadhi ya Watanzania Wamezaliwa Kuchukia wakiona Watanzania Wenzao Wanafanikiwa na Kuipa Sifa Nchi…ila hao niachieni Mimi, Nitadeal nao…na Round hii watashusha Viingilio Mpaka viwe shilingi Mia !!…Wambie Jumamosi Dec 7 naujaza Uwanja wa GUINÉ BISSAU… Dec 20th Uwanja wa DOUALA CAMEROON…. half Tareh 25 Dec Naujaza Uwanja wa LAKE TANGANYIKA Stadium KIGOMA!…waje tena kisirisiri kujifunza, kama Walivyokuja ya Dar”

View this post on Instagram

Mama See how much SIERRA LEONE Loves your Son😭😭😭.... 70,000+ STADIUM #SOLDOUT Last Night!.... i can't even Explain how Grateful i am SIERRA LEONE 🇸🇱❤🇸🇱..... GUINNÉ BISSAU we fill LINO CORREIA STADIUM this Saturday Dec 7th🙏🏼.... CAMEROON Douala National stadium Dec 20th 🛸🌍🛸 Kuna Baadhi ya Watanzania Wamezaliwa Kuchukia wakiona Watanzania Wenzao Wanafanikiwa na Kuipa Sifa Nchi...ila hao niachieni Mimi, Nitadeal nao...na Round hii watashusha Viingilio Mpaka viwe shilingi Mia !!...Wambie Jumamosi Dec 7 naujaza Uwanja wa GUINÉ BISSAU... Dec 20th Uwanja wa DOUALA CAMEROON.... half Tareh 25 Dec Naujaza Uwanja wa LAKE TANGANYIKA Stadium KIGOMA!...waje tena kisirisiri kujifunza, kama Walivyokuja ya Dar🙏🏼 #SIMBAinSIERRALEONE #SIMBAinFREETOWN #Afrobeats #Africa #Wcb4Life #Sierraleone #Freetown #WestAfrica #Tanzania #DiamondPlatnumz #Simba #Africa #Babalao #YopeRemix #SoundDp #Inama #YopeChallenge #Tetema #SIMBA

A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on



Sasa baada ya Fiesta kufanyika wikiendi hii ambayo ilikuwa tarehe 8 mwezi wa 12 na kufanikiwa kujaza sana tena katika uwanja mkubwa kuliko uwanja lilikofanyika Tamasha la Wasafi Festival maneno yameanza mitandaoni tena hadi kupelekea msanii Nay Wa Mitego kutupa dongo kwa Diamond na kumwambia kuwa

“Nasikia BabaTiffa Unasema Eti Fiesta Haikujaa.? Nakujua Mwanangu Ukipanic Huwa Unakua Na Tatizo La Kuona, Sasa Relax Chukua Time Yako Tizama Hii Clip Kwa Dakika 1 Tu, Haija Editiwa Ata Ata Kidogo Utapa Jibu Na Utaendelea Na Kazi Zako Zingine😂. Pia Nikukumbushe Kitu, Mtoto Ni Mtoto Na Mama Ni Mama Tu.”