Mtangazaji na muigizaji maarufu bongo, Mwijaku ameutaka uongozi wa WCB kuacha kutafuta huruma za watanzania kwa kuzusha mambo na wasitangaze kuwa wameonewa na Clouds Media wakati wao wenyewe walikataa nyimbo zao zisipigwe na kituo hicho bila kukumbuka fadhila za Marehemu Ruge kwani ndio kawaweka mahali walipo kwa kuwafungulia njia za kimuziki kama kufanya matamasha makubwa ndani na nje ya nchi na kolabo za nje, aliongeza kwa kufichua kuwa hata kolabo ya Davido na Diamond ilitokea sababu ya Clouds hivyo wasijione wamefika na kusahau walipotoka na kuanza kuwarushia vijembe watu ambao walikuwa msaada mkubwa kuwafikisha mahali walipo kwa sasa.