Mtangazaji wa Classic Fm, Mwijaku ambaye pia ni mwanafamilia wa Clouds, amefunguka kuwataka viongozi wa WCB kuacha kuomba huruma kwa Watanzania kwamba wanaonewa na Clouds Media wakati wao ndio walikataa nyimbo zao sipigwe na kituo hicho.

Akaenda zaidi na kusema kuwa wasijitape sana kwani Clouds na Marehemu Ruge ndio wamewaweka mahali walipo kwa kuwafungulia njia kwani Diamond na uongozi wake walikuwa wakishinda THT kuomba Connection za Collabo za nje...Hata ya Davido ilitokea sababu ya Clouds...Hivyo wasijione wamefika, Watanzania wakiamua wanaweza kuwashusha