Takriban watu 26 nchini Mongolia wamepoteza maisha yao tangu mwanzo wa Desemba kutokana na sumu ya pombe katika mji mkuu wa Ulaanbaatar.
Kwa mujibu wa mkuu wa sekta ya kuzuia majanga nchini humo Lkhamaa Amarmurum, unywaji wa pombe umeongezeka katika mji huo kutokana na sherehe za mwaka mpya.
Maafisa wa polisi wa Ulaanbaatar wamekuwa makini mwezi huu kwa janga lolote litakalotokea.
Huu mwezi, mashirika mengi ya umma na ya kibinafsi wanaendeleza sherehe zenye vyakula na vinywaji vingi vya pombe katika migahawa na vilabu ili kukaribisha mwaka mpya.