Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wananchi wa vitongoji vya Mwanubi, Magunguli na Kolandoto, kwenye ofisi cha Chama zilizopo Kata ya Kolandoto.
Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele, amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anyoifanya ya kusimamia nidhamu ya fedha na watumishi wa umma, hali ambayo imesukuma kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo.
Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) amebainisha hayo leo Desemba 27, 2019, katika mfululizo wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake la Shinyanga mjini na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Amesema kutokana na kazi nzuri ambayo anaifanya Rais John Magufuli ya kusimamia nidhamu ya fedha na watumishi wa umma, kazi yake imeonekana, ambapo miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa, kitendo ambacho kimezidi kukiimarisha chama cha Mapinduzi na kuwa na imani kwa wananchi.
Masele amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli uchaguzi mkuu mwaka 2020 CCM itashinda kwa kishindo kama ilivyofanyika uchaguzi Serikali za mitaa mwaka 2019.
“Nampongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia nidhamu ya fedha, na mimi Mbunge wenu nitaendeleza kasi hii ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama anavyofanya Rais wangu, nadhani mnaiona Shinyanga jinsi ilivyobadilika kimaendeleo kwa sasa ndani ya miaka yangu tisa ya ubunge, ambapo kuna barabara za lami kila mtaa, pamoja na taa zake,”amesema Masele.
“Huduma za afya nimeziboresha, elimu, maji yapo, ujenzi wa madaraja, na sasa hivi tumeshatenga tena kilomita 18 za ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami tofauti na hizi Kilomita 13 ambazo zimejengwa, yaani nataka Shinyanga uwe Mji wa kisasa ninaposema Shinyanga ni Paris ya Tanzania nina maana kubwa ya kuifanya shinyanga kuwa pahala pazuri pa kuishi kama ilivyo miji ya kisasa. Na uwezo huo ninao,”ameongeza Masele.
Pia ameahidi kuendelea kumalizia baadhi ya ahadi zake ambazo amebakiza kwenye baadhi ya maeneo, huku akitoa mifuko ya Saruji 150 ili kumalizia majengo ya ujenzi wa Zahanati ya Mwanubi, ambapo wamepatiwa mifuko 100 ya Saruji, pamoja na zahanati ya Mwamagunguli Mifuko 50 zote za Kata ya Kolandoto ili kusogeza huduma za afya kuwa karibu na wananchi.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata hiyo ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga akiwemo Naimani Ngeleja, wamempongeza Mbunge Masele kwa kazi nzuri ambayo ameifanya kwenye uongozi wake, ikiwa ahadi nyingi amezitekeleza huku wakiomba awasaidie kupeleka huduma ya umeme wa REA kwenye baadhi ya vijiji ambavyo havijapitiwa na mradi huo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kolandoto Agnes Machiya, akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kuanzia (2015-19), amesema asilimia 90 ya ahadi zimeshatekelezwa, ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, elimu, Afya pamoja na miradi ya maji safi na salama.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele, akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Galamba Kata ya Kolandoto akiwa kwenye ziara yake leo Desemba 27,2019. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele, akizungumza katika kitongoji cha Galamba Kata ya Kolandoto.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wananchi wa vitongoji vya Mwanubi, Magunguli na Kolandoto, kwenye ofisi cha Chama zilizopo Kata ya Kolandoto.
Diwani wa Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ya kata hiyo kwenye ziara ya Mbunge Masele.
Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Rashid Mnunduma, akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa kamati wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini, wakiwa wameambatana na mbunge Masele kwenye ziara yake.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Galamba Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Galamba Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Galamba Kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Mwanubi, Magunguli na Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Mwanubi, Magunguli na Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Mwanubi, Magunguli na Kolandoto manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mbunge Masele.
Mwananchi Naamani Ngeleja ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho akimpongeza Mbunge Masele kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kutekeleza ahadi zake.
Bulugu Mboje ambaye alikuwa akigombea nafasi ya uenyekiti wa kijiji Galamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akirudisha kadi na kujiunga CCM ili kuunga juhudi za Rais John Magufuli, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akimkaribisha Bulugu ndani ya CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akimkaribisha CCM Bulugu Mboje ambaye alikuwa akigombea nafasi ya uenyekiti wa kijiji Galamba kupitia CHADEMA.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele, akisalimiana na mgonjwa alipofika kutembelea zahanati ya Galamba.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele, wa kwanza wa kulia, akisikiliza maelezo ya Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Galamba Manyasi Janeti, mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa maabara kwenye Zahanati hiyo.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.