Kuna tuhuma tatu kuhusiana na muonekano wa bendera hiyo, tutawaorodhesha hapa tuhuma hizo na kuzichambua.
Tuhuma ya kwanza inasema:
-Watu wa Kigoma ni washamba na hawajasoma, Bendera inayo onekana hapo ni bendera ya nchini Uingereza (United Kingdom) iweje ipeperushwe na ilihali wana Kigoma sio waingereza?
#JAWABU
Bendera hiyo siyo ya nchini uingereza na wala haina unasaba na uingereza, kumbuka bendera ya uingereza imeundwa kwa mfumo wa (Union Jack) yaani mistari yote imekutana kwenye msaraba mwekundu, lakini hii iliyoonekana imeundwa kwa mfumo wa (Union face) kwa maana katikati ya bendera kuna picha ya mlengwa ambae ni Diamond ikimaanisha watu wameungana na kukusanyika kwa ajili yake, na wala hakuna msaraba mwekundu kama bendera ya UK.
Tuhuma ya pili inasema
-Bendera inayoonekana ni bendera ya kishetani inayomilikiwa na Freemason huko Kigoma na ndio imekusanya nguvu ya watu hao.
#JAWABU.
Si kweli, kwasababu bendera ya freemason haiko union, yenyewe ina rangi ya Blue na Njano au Blue na Gold Compass Masonic Flag. Nasio hii iliyoonekana hapa Kigoma. Ni kweli mnamo sep 5, 2017 kijana Emmanuel Songoye aliuwawa kwa kuchomwa moto na wananchi huko Kabanga, kasulu akihofiwa kuwa ni Freemason kutokana na mali zake, lakini haina uhusiano wowote na bendera hii hata kidogo.
Tuhuma ya tatu inasema
-Bendera inayoonekana ni bendera ya kichawi iliyokuwa ikiwaongoza watu bila kujijua kwa maana watu wote walionyoosha mikono juu pia walifungua viganja vyao vya miko (yaani vidole vyote vya mikono vilikunjuka kwa watu wote),
#JAWABU
Si kweli, hii bendera haijatumika kama ushirikina au uchawi kuongoza watu, mkumbuke wakati watu wananyoosha mikono juu walikuwa wakiimba kwa kuwapungia mikono wasanii waliokuwa upande wa jengo la station ghorofani, sasa kikawaida huwezi kumpungia mtu mkono ilihali umekunja ngumi, ni maswala ambayo hayaingii akilini.
UHALISIA WA BENDERA
Bendera hii imechorwa kama bendera ya ulaya 'United Kingdom' kwa maana ya muonekano wa rangi zake, kwakuwa Kigoma iliungana kumpokea Diamond basi hakuna budi kuitwa ''Kigoma United for Diamond Platinum'' au unaweza kuita ''United Kigoma'' badala ya ''United Kingdom''. Mchoraji ameondoa Kingdom na kuweka Kigoma kwasababu katikati ya bendera ameweka picha halisia ya msanii Diamond Platinumz.