Kampuni inayomilikiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva @diamondplatnumz ZOOMPRODUCTION yabadilishwa jina na muonekano wa logo ya utambulisho

Kampuni hiyo inayojihusisha na utayarishaji wa video za muziki na matangazo kwa sasa inaitwa Zoom Extra na si Zoom production kama ilivyokuwa hapo awali. Hata muonekano wa Logo inayobeba utambulisho wa kampuni pia imebadilishwa

Hapo awali kampuni hii ilisemekana kumilikiwa na Diamond & Harmonize ambaye alikuwa mwanachama wa lebo ya WCB. Hivyo kuondoka kwa Harmonize WCB kunatajwa kuwa moja ya sababu ya kusitishwa kwa biashara kati ya Harmonize na Diamond juu ya Zoom Production na hivyo Harmonize ameamua kuondoa hisa zake kwenye kampuni hiyo na Diamond amebaki kuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo.