Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda, akizungumza na watumishi wa Tanapa katika -Hifadhi ya Ruaha mkoani Iringa pamoja na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani )waliohudhiria hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya doria kutoka mradi wa REGROW kuimarisha Uhifadhi na Kukuza Utalii

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda koine mbali(darubini) kutazamia Wanyama.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda Akitoka kwenye moja hema katika Hifadhi hiyo ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda akikagua vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na mahema, mabegi, vifaa vya kukusanyia taarifa (camera, GPS), sare, magodoro, buti, vifaa maalumu vya kufanyia doria usiku na vinginevyo vyote vikiwa vimenunuliwa kupitia mradi wa REGROW.


Na Vero Ignatus, Ruaha
KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amewataka watanzania kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio makubwa yanayofikiwa katika sekta ya utalii kwa kuwekeza kwenye sekta hiyo ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 1.2 bilioni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Kwa Hifadhi nyingine zilizoko chini ya mradi wa REGROW.

Amesisitiza kuwa, ni vizuri kila mmoja kwa nafasi yake akaona umuhimu wa kushiriki kuitangaza nchi kupitia utajiri wa rasilimali iliyojaliwa kuwa nayo jambo ambalo litakuwa na mchango katika ukuaji wa sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla.

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na Mahema, Vifaa vya kukusanyia taarifa (camera, GPS), sare, magodoro buti, vifaa maalumu vya kufanyia doria usiku na vinginevyo vimenunuliwa kupitia mradi wa REGROW.

Awali, Mratibu wa Mradi wa REGROW Saanya Aenea amesema serikali kupitia mradi huo imedhamiria kumaliza changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikabili hifadhi katika ukanda wa kusini mwa nchi na hasa eneo la miundombinu.

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha inapatikana kwa sehemu kubwa mkoani Iringa na ni ya pili kwa ukubwa ikiwa na kilomita za mraba zaidi ya elfu 20