Mtambo wa Transfoma uliozinduliwa leo na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani yenye uwezo wa kuzalisha umeme MVA 300 sawa na MW 240 wenye thamani ya Bilion 13.3

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema kuwa kumaliza kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ubungo kitaondoa changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika kwa muda mrefu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuimarisha upanuzi wa miradi kwa kujenga transfoma mpya yenye uwezo wa kuzalisha umeme MVA 300 sawa na MW 240 wenye thamani ya Bilion 13.3 ambapo itachangia kuboresha upatikanaji wa umeme kwa wingi na kuchochea sekta ya Viwanda.


Kalemani amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo Jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa kukamilika kwa mradi hu ndani ya wakati kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kupelekea shirika kupata maata mengi zaidi.


Amesema, mahitaji ya mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa ni ni MW 592 na kabla ya kukamilika mradi huo transoma zilikuwa zinazalisha umeme MW 577 na kupelekea ukosefu wa umeme kwa baadhi ya maeneo na kushindwa kukidhi mahitaji ya wananchi hususani muda transfoma moja inapkuwa inafanyiwa matengenezo.

"Transfoma hii ni kubwa na inazalisha MVA 300 sawa na MW 240 ambapo ukijumlisha na MW 592 tunapata jumla ya MW 817 na kupelekea kubakiwa na umeme mwingi wa akiba, ambapo tunaweza kuwapatia Mikoa mingine kama Morogoro, Kilimanjaro  na Tanga,"amesema Kalemani.

"Sasa Tanesco mna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wananchi hawakosi umeme,mfanyie marekebisho miundombinu yote ya kusafirishia umeme ikiwemo transfoma, nyaya za umeme zilizochakaa,"

Pia, amewataka Tanesco kuongeza mapato kwa wiki kutoka Bilion 46 kwenda mbele zaidi baada ya kukamilika kwa transfoma hiyo.

Amesema, maeneo mengi ya Mkoa wa Pwani yalikuwa yanapata changamoto ya upatikanaji wa umeme na kule ndio Viwanda vingi sasa nawaagiza Tanesco muende kuwatembelea na muwahakikishie kuwa umeme upo wa kutosha sasa.

Kalemani amewapongeza Menejimenti ya Tanesco na Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti Dkt Alexandra Kyaruzi kwa kusimamia mradi huu kukamilika kwa wakati tena kwa siku tano kabla ya makubaliano ya mkataba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco , Dkt Kyaruzi ameishukuru serikali kwa kuwezesha kufanikisha mradi huu ambapo unaenda kuonda changamoto ya umeme ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo awali walikuwa wanashindwa kugawa umeme maeneo mengine kwa sababu haukuwa unatosheleza ila baada ya kumalizika kwa mradi huu anaamini maeneo yote haya yatanufaika.

Meneja mwandamizi usafirishaji umeme Tanesco, Amos Joas amesema, gharama za mradi huo ni bilioni 13.3 ambazo ni fedha za ndani za Tanesco na ulianza utekelezaji wake Septemba 24, 2018 na utekelezaji wake ukiwa ni miezi 15 chini ya mkandarasi ABB wa Switzerland na umeweza kusimamiwa kwa ufanisi mkubwa hadi kukamilika kwake.

Amesema, transfoma imeshaanza kufanya kazi na wapo katika kuangalia ufanisi kwa transfoma wakati imebeba mzigo ambapo manufaa yake yataimarisha na kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuimarika kwa kituo cha kupoza umeme chha Ubungo kwa kupokea na kugawa umeme mwingi zaidi, nyingine ikiwa ni kuwezesha kufanikisha matengenezo katika mitambo inayofua umeme na kuongeza mapato kwa serikali.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akitoammaagizo kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) baada ya kuzindua mradi wa  upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ubungo kitakacho zalisha umeme MW 240 na kuondoa changamoto ya umeme kwa muda mrefu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja mwandamizi usafirishaji umeme Tanesco, Amos Joas  akielezea utekelezaji wa mradi huo uliokamilika ndani ya wakati na umegharimu Bilion 13.3 zikiwa ni fedha za ndani za Tanesco.
Meneja mwandamizi usafirishaji umeme Tanesco, Amos Joas akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika chumba maalumu cha kuendeshea au kudhibiti mfumo wa umeme.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco , Dkt Alexandra Kyaruzi ameishukuru serikali kwa kuwezesha kufanikisha mradi huu ambapo unaenda kuonda changamoto ya umeme ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.