Moja kati ya stori ambazo zinazungumziwa kwa sasa katika mitandao ya kijamii hasa wa Instagram, ni msanii Hamisa Mobetto, kujizawadia gari aina ya Land Rover katika 'birthday party' yake iliyofanyika siku ya Disemba 14, 2019 Jijini Dar Es Salaam.


Wapo baadhi ya mashabiki ambao wanasema gari hilo sio lake, wengine wanasema amehongwa na amefanya kiki ili shughuli yake izungumziwe, huku wengine wakitaka waonyeshwe kadi ya gari na ataje gharama ya gari hilo.
Sasa kupitia insta stori ya mtandao wa Instagram, Hamisa Mobetto, alitupa vijembe kwa watu wanaombeza kuhusiana na kujizawadia gari hilo ambapo aliandika.

"Msijali mtakuwa sawa halafu kadri siku zinavyoenda mtazoea, kila mtu ashinde mechi zake hakikisha za mwenzako hazikupi mawazo 'stress', ameandika Hamisa Mobetto.

Ikumbukwe tu hata kwenye siku ya kuzaliwa kwa Mama yake Mzazi, Hamisa Mobetto, ambayo ilikuwa Oktoba 23, 2019, alimzawadia gari aina yaAlphad.

Kwenye birthday party hiyo ilihudhuriwa na mastaa kama Irene Uwoya,Tunda, Whozu, Official Nai, Irene Paul na Mwijaku.