Inaokeana kama msanii na mkurugenzi mtendaji wa Wasafi Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) amerusha dongo kwa waandaji wa show ya Fiesta iliyofanyika jijini Dar es salaam jana
Kauli ya Diamond kwenye mtandao wa Instagram imewashtua wengi na kuanza kutoa maoni tofauti juu ya kauli hiyo
Diamond ameandika
“Majukwaa yakijaa yanaletaga Mizuka ya Show jamani….Hasa Camera ikizungushwa kama Alivyofanya @lukambaofficial hapo….Sasa wewe @ricardomomo yanini Kung’ang’ania Ndoo ya lita 20 wakati uwezo wako ni kujaza kidumu cha Lita tano….Matokeo yake unaanza piga video na picha za Upande upande….. Dah! mie sina cha kukusaidia tena, maana Busta nilikupa na bei ukashusha, ila naona mnh! wananchi wamegoma Mwenzangu”
Huku akiwa ameposti kipande cha video ya show yake ya hivi karibuni ya nchini Sierra Leone