Vijana wawili wa Kanisa  la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam, Mhitimu wa Shahada ya kwanza katika udaktari wa binadamu,  Barbara James (kushoto) na Mhitimu Shahada ya kwanza katika Ufamasia,  Neema Luvanda wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu 21 wa mafunzo ya awali ya uongozi katika  kanisa wa kanisa hilo kwenye mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika jana.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mahafali yakiendelea.
 Mtumishi wa Mungu, Martin Milyango akiwa kwenye mahafali hayo. 
 Mahafali yakiendelea.
 Mahafali yakiendelea.
 Mahafali yakiendelea.
 Mahafali yakiendelea.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, akimpongeza mke wake Janeth Ndabila kwa kuhitimu mafunzo hayo.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, akiwapongeza wahitimu wa mafunzo hayo.
 Katibu  wa Kanisa la ABC, Peter Sifi, akizungumza na wahitimu hao.
 Mzee wa kanisa hilo, Jane Magigita akizungumza na wahitimu hao.
 Mke wa Askofu Mkuu wa Makanisa  ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, Janeth Ndabila akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa.
 Vijana wawili wa Kanisa  la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam, Mhitimu wa Shahada ya kwanza katika udaktari wa binadamu,  Barbara James (kushoto) na Mhitimu Shahada ya kwanza katika Ufamasia,  Neema Luvanda wakikata keki.
 Mzee wa kanisa hilo, Jane Magigita, akilishwa keki.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake wakiwalisha keki wahitimu hao.
 Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
 Vijana wa kanisa hilo, wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
 Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila  na mke wake Janeth Ndabila wakiwa na wahitimu hao wa shahada za kwanza za udaktari na ufamasia.
Wahitimu hao wakitoka kwenye mahafali hayo.

Na Dotto Mwaibale

CHUO cha Biblia cha Kanisa  la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kimetoa wahitimu 21 wa mafunzo ya awali ya uongozi katika  kanisa.


Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana,  Askofu Mkuu wa Makanisa  ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila alisema hayo ni mafanikio makubwa sana ya kanisa hilo.

"Baada ya kipindi cha miaka 25 ya huduma ya kanisa letu tumefanya mengi lakini tukaona sasa na sisi tuanzishe chuo chetu cha biblia kwa ajili ya kufundisha uchungaji na kuwanoa wachungaji waliopo makanisani wakiendelea kutoa huduma" alisema Ndabila.

Alisema wanamshukuru Mungu kwa kufanya mahafali yao ya kwanza ambayo yalikwenda sanjari na kuwapongeza vijana wawili wa kanisa hilo kwa kufanikiwa kupata  shahada ya kwanza katika udaktari wa binadamu kwa Barbara James na Shahada ya kwanza katika Ufamasia kwa Neema Luvanda.

Ndabila alisema lengo la kuanzisha chuo hicho ni kutaka kupata wachungaji wasomi ambao watakwenda na wakati kutokana na mabadiliko makubwa ya elimu, kiuchumi na teknolojia na ukuaji wa kanisa.

Alisema wanafunzi walioanza masomo hayo walikuwa 24 lakini watatu kati yao waliishia njiani kutokana na sababu mbalimbali na waliohitimu na kukabidhiwa vyeti walikuwa 21 wanaume wakiwa 14 na wanawake 7.

Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ambaye ni Katibu  wa Kanisa la ABC, Peter Sifi aliwataka wahitimu hao kwenda kutumia elimu waliyoipata kutoa majibu kwa watu watakao kuwa wanawatumikia.

"Elimu mliyoipata ikatoe majibu kwa watu ambao mnaenda kuwatumikia na kuonesha tofauti kati ya ninyi mliobahatika kusoma na wale ambao wamekosa bahati hiyo" alisema Sifi.

Alisema dunia hivi sasa imebadilika kwa mambo mengi hivyo wanahitaji wasomi kusaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo kazi ya kanisa.