Mwanamziki Christian Bella ambaye anafanya poa sana kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva amekiri kuwa yuko mbioni kuomba uraia wa Tanzania. 

Bella ambaye kwa sasa makazi yake ni Tanzania katika jiji la Dar es Salaam amesema hayo wakati wa uzinduzi wa video ya  kibao chake kipya alichofanya na Alikiba inayokwenda kwa jina la CHAKU.

 Bella amesema kuwa anakila sababu ya kuomba uraia wa Tanzania kwa kuwa ni mahali ambapo ameweza kujitengenezea jina lake.

 “Mimi ninaishi na kibali cha makazi tangu naingia Tanzania, isitoshe vigezo vya kupata uraia ninavyo hivyo ukifika muda muafaka nitajisajili, pia kuna sababu kubwa ya kufanya hivyo kwa kuwa Tanzania imenipa jina na ikifika muda mitaweza kujisajili, lakini hadi sasa bado ninaishi kama mkazi wa kudumu” ameongeza Bella.

 Safari ya Christian Bella kimuziki nchini Tanzania ilianza mwaka 2006 baada ya kuingia nchini na kujiunga na Akudo, ambapo wimbo wake wa kwanza kutanga ulikuwa ni “Walimwengu si Binadamu” uliyofatwa na “Yako wapi Mapenzi”.

Hata baada ya kuachana na bendi ya Akudo mwaka 2003 Bella aliamua kuanzisha bendi yake ya Malaika ambayo anafanya nayo kazi hadi sasa.

Christian Bella ambaye alishwahi kufanya kazi na Alikiba taribani miaka mitatu iliyopita ambapo wawili hao walikuja na kibao “Nagharamia”. Ambapo Bella amekiri kuwa kufanya mziki na Alikiba ni jambo ambalo analifurahia kwa kuwa wawili hao wanaendana.

Bella pia ameongelea kuhusu kufanya kazi na wasanii wa kike ambapo amewataja wasanii kama Rosa ree pamoja na Nandy kuwa ni wasanii ambao anatamani kufanya nao kazi.