Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid ametuma ujumbe wa kumtaka Staa wa muziki wa Singeli nchini Tanzania, Dullah Makabila kaundaa wimbo (verse) waje kufanya wote.

Wizkid alimtumia ujumbe huo kwenye mtandao wa Instagram, baada ya Dullah kumkaribisha Tanzania Staa huyo wa wimbo ‘Joro’ anayetarajiwa kutoa burudani ya aina yake kwenye jukwaa la Wasafi Festival, Nov. 9 mwaka huu.

Tamasha hilo litakalofanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam katika viwanja wa Posta Kijitonyama litawakutanisha wakali kibao wa ndani na nje ya Tanzania na Staa Mwingine kutoka Nigeria, Tiwa Savage.