Msanii wa Bongo Fleva, Whozu amesaini mkataba na kampuni ya Too Much Money inayoongozwa na kaka yake Frank pamoja na Fred yenye ofisi zake Guangzhou, China.

Mkataba huo unahusisha Kusimamia kazi za Muziki, vichekesho pamoja na biashara ambazo zitahusisha jina la msanii huyo ambapo amelipwa zaidi ya Millioni 60 za kitanzania.

Pia akiwa China, Whozu amefanya kazi mbalimbali ikiwemo kurekodi nyimbo na Producers wa China wenye asili ya Nigeria pamoja na kufanya video tatu.