Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amemtaka msanii wa miondoko ya HipHop nchini kuachana na muziki kama ataendelea kuikosoa serikali.
Kauli ya Mwakyembe imekuja kutokana na Roma kuachia wimbo juzi unaojulikana kwa jina la Anaitwa Roma aliomshirikisha One Six.
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa.
"Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi.
"Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa."