VIDEO ya wimbo UNO wa msanii Harmonize umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya mtayarishaji Magix Enga wa nchini Kenya kulalamikia matumizi ya wazo la wimbo aliotayarisha uitwao Dundaing wa King Kaka feat. Kristoff.

Kupitia ukarasa wake kwenye mtandao wa Instagram Magix alisema “Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪.” Wimbo huo Dundaing unaidaiwa kuigwa na Harmonize ulitoka miezi 12 iliyopita.