KILA mtu na aina yakeya maisha, lakini huko Instagram wapo watu wanakupangia hadi mwili wako uweje.

Hiyo imemtokea staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambapo amedaiwa kuwa amekuwa bonge kupitiliza hivyo apungue.

Kwenye ukurasa wa Instagram, mtu anayejiita betting_tips_222, alitupia picha ya hivi karibuni ya Shilole na kumtaka apungue ambapo alimshauri amuige Wema ili angalau kidogo mwili uwe na mvuto. “Mwambie Wema Sepetu akupe darasa

usione aibu umekuwa kama jaba la kutunziamaji ya mvua,” aliandika betting_ tips_222 lakini hata hivyo Shilole hakumjibu chochote licha ya kipande hicho kusambaa kwenye kurasa nyingi za watu Instagram.