DUNIANI kuna vituko! Video queen maarufu Bongo, Anna Kimario ‘Tunda’ ametoa kali ya mwaka kwamba ukimya wake unatokana na betri yake kuzima chaji na sasa anaichaji ili aweze kusikika tena.  Akibonga na Za Motomoto News, Tunda alisema kuna kipindi lazima watu wakusahau kidogo kisha waanze kukukumbuka tena, hivyo kwa upande wake betri yake ilitumika sana na kuzima chaji. Kwa hiyo anaichaji.

“Unajua ni lazima ufike wakati betri ichajiwe upya ili kama ni gari au simu ishike kasi mpya, kwa sababu bila hivyo vitakufa na kuzima kabisa. Hivyo, mimi siyo kwamba nimezima moja kwa moja, bali najichaji na hivi karibuni tu mashabiki watanisikia tena,” alisema Tunda.