EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii wa mashairi Mrisho Mpoto, ambaye amefunguka kuhusiana na kutoimba nyimbo za mjomba kama ilivyokuwa katika utawala wa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na suala la kuingia kwenye siasa kama watu wanavyotaka kumuona huko.




Kuhusu kutoimba nyimbo za 'Mjomba' katika utawala huu wa Rais Dkt Magufuli, Mrisho Mpoto amesema.

"Muda bado ndiyo kwanza ameingia, labda tunaandika hamuwezi kujua ndiyo kwanza ana miaka minne tujipe muda, wote kwa sababu hizi kazi hatuandiki kwa ajili ya mtu unaandika kwa sababu ya 'passion' kwa hiyo tujipe muda" ameeleza Mrisho Mpoto.

Aidha akizungumzia suala lake la matarajio ya watu wengi kumuona akiingia kwenye siasa, Mrisho Mpoto ameeleza kuwa,

 "Labda wakati bado, tusubiri wakati umri si bado upo,  wakati ukifikia mahojiano kama haya yatahusika, nafasi itakayonifaa labda ni ujumbe wa nyumba kumi"  amesema.