Na Chalila Kibuda,Morogoro

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  amesema kuwa Wananchi wote watasajili laini za simu kwa alama za vidole kutokana na jitihada walizoweka kwa kushirikiana na wadau katika kufanikisha usajili huo.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro, Odiero amesema zoezi la elimu pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole linafanyika katika mkoa wote wa Morogoro kwa kupita kila Kata.

Amesema katika utoaji wa elimu wanashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Watoa Huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi ,Wakala wa Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA) kwa kupata Wananchi huduma kwa pamoja.

Amesema Wananchi watumie muda wao kutafuta viambatanisho vinavyohitajika kwa wadau wengine ili waweze kusajili laini zao kwa alama za vidole.Katika utoaji elimu hiyo wamepita katika vituo vya radio vya Mkoa wa Morogoro kutoa elimu hiyo watu kujitokeza kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema utoaji elimu unakwenda katika mikoa yote iliyopo katika kanda ya Mashariki ambapo zoezi hilo lilishamalizika katika Mkoa wa Pwani na kutaka Wananchi wa Mkoa huo ambao hawana vitambulisho vya Taifa kufanya utaratibu wa kupata katika Ofisi za NIDA ili waweze kusajiliwa.
Kwa upande mwananchi Amina Salumu wa Manispaa ya Morogoro amesema TCRA wamefanya vizuri kuhamasisha kwa kuungana na watoa huduma wote  katika usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema kuwa tatizo lingine ni wao Wananchi kushindwa kufuata taratibu za kuweza kupata vitambulisho kwa wakati kwa kizingizio cha majukumu yao.

Salumu ameshauri kuwa zoezi hilo lifanyike mara kwa mara ili wote waweze kujisajiliwa wasisubiri laini zifungwe ndipo waanze kuhangaika.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero aliyesimama akiangalia kazi data waliosajiliwa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya Namba waweze kujisajili laini za simu kwa alama za vidole katika utoaji wa elimu katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
 Wananchi wakisajili laini za simu kwa alama za vidole kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu katika utoaji elimu  Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaoleth Esseko akimkabidhi kitabu Cha mkataba kwa Wateja Cha TCRA wakati utoaji elimu Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.

 Mwananchi akisubiri kupewa namba ya kitambulisho cha Taifa kwa kuangalia mfumo aliyessjiliwa na NIDA.