Msanii wa filamu Single Mtambalike, amesema yeye sio mtu wa kiki kama walivyo wasanii wengine pia hataki kuburuzwa na wananchi kwa wanavyotaka wao kwenye kazi zake.


Akipiga stori  na EATV & EA Radio Digital, Single Mtambalike ameeleza kuwa tangu amechukua tuzo yupo kimya sio mtu wa kupiga kelele kama wasanii wanavyofanya  na hataki kuburuzwa na style zinazokuja.

"Ukisikia mtu amefanya kitu halafu anasema hivi na vile kama kuahidi vitu vinavyokuja halafu inakuwa kimya hamna kitu, lakini mimi tangu nimechukua tuzo nimekuwa hivi hivi na nimetoa filamu na tamthilia nipo hivi hivi kwa hiyo sitaki kuburuzwa na style zinazokuja hapa katikati nikazifuata halafu nikapoteza muelekeo wangu  " ameeeleza.

"Sitaki kufanya kitu na kuwaachia wananchi na sio kwamba nimechukua tuzo Nigeria iwe tabu mjini hapana" ameongeza.

Aidha Single Mtambalike amesema ili filamu ikamilike lazima izingatiwe vitu kama hadithi, "perfomance" ya watu, upigaji picha na sauti kwa ujumla hiyo ndiyo itakuwa filamu iliyotimia na zitapimwa na watazamaji.