mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo kwa mkandarasi mara baada ya kutembelea moja ya kisima cha maji ya mradi wa shilingi bilioni 520 kilichopo Ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo alimtaka mkandarasi kuhakikisha adi ifikapo November 30 wananchi wawe wameanza kupata maji.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba akimpa maelekezo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jinsi maji yanavyoingia katika tanki kubwa la lita milioni 10 ambalo limekamilika na jana november 24 zoezi la usafishaji mabomba kwa ajili ya matumizi ya binadamu ,tanki hilo kubwa lipo mji mdogo wa ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru maji haya ni ya mradi wa kiasi cha shilingi bilioni 520 uliotolewa na serikali na yatahidumia jiji zima la Arusha (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba akiongea na wakandarasi na wafanyakazi Wa AUWSA Mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa Wa shilingi bilioni 520.(picha na Woinde Shizza Arusha) .
Moja ya bomba la Maji likiwa linatoa Maji mengi wakati Wa kusafisha mabomba.

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha.

Serikali imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji Wa mradi mkubwa Wa Maji Wa shilingi bilioni 520 unaotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Arusha utakao hudumia wananchi .

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo ,Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji , Nadhifa Kemikimba alisema kuwa amerithishwa na kasi ya ujenzi Wa mradi huo huku akibainisha kuwa nia ya serikali nikuona hadi ifikapo mwaka 2020 upatikanaji Wa huduma za Maji kwa Mjini umefikia asilimia 95% huku vijijini wananchi wanapata Maji kwa asilimia 85%.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba alisema kuwa mradi huo umefikia hatua ya kusafisha mtandao Wa mabomba yanayopeleka Maji kwenye tanki pamoja na kuweka Maji dawa tayari kabisa kwa ajili ya wananchi kuanza kutumia.

"Kama ulivyoona tumepita katika matanki yetu ya Maji natumeona tanki moja la Lita milioni kumi tumeanza kuweka Maji kwani ujenzi Wa tanki hilo umekamilika hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ongezeko la Maji na tutaanza kuwapa wale wenye matatizo ya Maji kama muriet na olasiti" alisema Mwangijomba.

Akiongelea mradi huo Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa kuna ujenzi Wa makao makuu ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka ambao ulikuwa unasuasua lakini baada ya OFISI yake kwakushirikiana na msimamizi Wa mkandarasi kufatilia kwa makini ujenzi huo umeanza kwenda vizuri

Akibainisha kuwa walipotembelea mradi huo ujenzi ulivyokuwa ukisuasua ulikuwa umefikia asilimia 7.5 lakini baada ya kuusimamia vizuri umeongezeka na kufikia asilimia 10 ambapo alibainisha mbali nakufuatilia mradi huo pia wamempa mkandarasi mashariti ya kufanya Kazi usiku na mchana ,kuwasilisha taarifa za mradi unavyoendelea kila wiki huku akimtaka ajenge kwa kufuata vipimo vinavyotakiwa na katika ubora unaotakiwa 

Kwa upande wake Mkuu Wa wilaya ya Arusha alisema kwamba kumalizika kwa mradi huo kutawasaidia wakazi Wa jiji la Arusha kuondokana na tatizo la Maji.