Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.

Anthony Ishengoma -Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Sekta ya Afya Nchini inachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa Nchini kwa baadhi ya watoa huduma ya Afya kushiriki kuficha ushaidi kwa njia ya rushwa.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma ili kujenga uelewa kwa kamati ya Bunge kuhusu mpango huo.

Dkt. Ndugulile amesema watoa huduma ya Afya wanawajibu wanapopata zile kesi zinazohusiana na ukatili wa Kijinsia kuhakikisha wanazingatia miiko na misingi ya taaluma zao kuhakikisha hawawi sehemu ya kuvuruga ushaidi.

“Sisi kama Wizara tutakapobaini kwamba mtoa huduma wa Afya yoyote atakayeshiriki katika katika kosa la kuvuruga ushaidi kwa waanga wa ukatili wa kijinsia hapa Nchini tutamfutia lesseni ya kufanya kazi ya kutoa huduma za Afya katika Nchi yetu’’. Aliongeza Dkt. Ndugulile.

Pamoja na masuala ya ukatili wa Kijinsia Dkt. Ndugulile amesema pia vijana wengi wanaanza kujamiina wakiwa katika umri mdogo na kwa mjibu wa takwimu za masula ya ukimwi za mwaka 2017 zinaonesha asilimia 40 ya Watanzania ni vijana na kati hao mabinti peke yake ni 80%.

Kufuatia hali hiyo ya vijana kujihusisha na masuala ya kujiimiana Dkt. Ndugulile amesema serikali inakusudia kupeleka Sheria Bungeni ili kupunguza umri wa vijana kuanzia miaka 15 kupima umri kwa hiari lakini pia kujipima wenyewe na kuweza kujilinda lakini pia kulinda wenzi wao.

Aidha Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa sheria iliyopo inasema mtoto chini ya umri wa miaka 18 harusiwi kupima virusi kwa hiari labda kwa ruhusa ya mzazi wake lakini wiki ijayo Wizara inapeleka bungeni mabadiliko ya sheria ili suala la kupima virusi kwa hiari lianze kufanyika mpaka umri wa miaka 15 kwa kuwa watoto sasa wanaanza kujiamiina katika umri huo na bila idhini ya wazazi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Takwimu za Viashiria vya Hali ya Afya Nchini zinaonesha kwamba kati ya 27% ya mabinti walio katika umri wa miaka 15-19 mmoja kati ya watatu ama ni mjazito au ana mtoto hii inatoa picha kwamba watoto hawa wanaanza ngono katika umri mdogo ndio maana serikali inatoa chanjo ya kansa ya mlango kizazi kwa watoto wa kike wenye umri huo lakini pia sula limepelekea kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili wapime virusi kwa hiari.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba amewataka Wajumbe wa Kamati yake kuwa mabarozi wa masuala ya ukatili wa Kijinsia Nchini ili masuala hayo yaweze kupewa kipaumbele katika Bajeti za Wizara mbalimbali Serikalini.

Pamoja na maoni yake hayo Bw. Serukamba ameyataja matendo ya ukatili kuwa yamekuwepo kwa mingi lakini Jamii kama zilivyo mila na desturi zetu imukuwa ikifanya vitendo hivyo kwa usiri tofauti na wenzetu wa Nchi za Magharibi ambapo watu wanajitangaza hadharani kuwa ni wao ni mashoga na wanaweza kujitokeza hata kugombea nafasi za juu katika uongozi.

Aidha kiongozi huyo wa Bunge ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali lakini haitoshi tu kutokomeza matendo haya hivyo kuitaka Wizara pamoja na wadau kutoa elimu ya kutosha kwa umma ikiwemo adhabu kwa wote wanaohusika na makosa haya kupewa adhabu kali.

Bw. Serukamba ameutaja umasikini kuwa sababu mojawapo ya kuchochochea ukatili wa kijinsia kwa wanawake kwa kuwa baadhi ya wanawake wanakubali kunyanyaswa kwasababu ya umasikini wa kipato na utegemezi hivyo kukubali kupigwa au kuonewa kwa namna mbalimbali.

Semina ya wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) imemalizika leo Jijijini Dodoma na imelenga kujenga uelewa kwa kamati ya Bunge kuhusu masuala ya ukatili na mpanga mkakati huo wa miaka mitano unaotegemea kukamilika mwaka 2022.