Mkufunzi Mkuu wa Karate Mkoa wa Singida, Salum Musa (kushoto), akifanya mazoezi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa kilele cha kufunga wiki ya Maadhimisho ya Magonjwa Yasio ya Kuambukiza yaliyofanyika viwanja vya Bombadia mjini hapa jana. 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (katikati) akifanya mazoezi.
 Wanafunzi wakifanya mazoezi.
 Mwalimu Juma Mataka kutoka Manispaa ya Singida, akiongoza mazoezi hayo.
 Afisa Utamaduni Mkoa wa Singida,  Henry Kapella, akiongoza kufanya mazoezi.
 Mazoezi yakiendelea.
 Mazoezi yakiendelea.
 Mazoezi yakiendelea. Kulia ni msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Singida, Mbwana  Mkingule.
 Mazoezi yakiendelea.
 Sister Maria Corola kutoka Mtiko, akipima uzito na urefu katika maadhimisho hayo. Katika  maadhimisho hayo kulikuwepo na huduma za upimaji wa afya kama, macho, kisukari, shinikizo la damu, urefu, na Ukimwi kwa usimamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sightsaver.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) akifanya mazoezi na Afisa wa Uhamiaji Mkuu wa Mkoa wa Singida, Safina Muhindi.
Mazoezi yakiendelea.
 Wauguzi kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine wakiwajibika kwa kupima afya za wananchi katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Consitancia Muua, Innocencia Paul na Lenicu Kilasi.
 Vijana wa Skati wakionesha ukakamavu.
 Muuguzi Catherine Msukuma kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, akimpima urefu Mwanafunzi Buruani Bashiri wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi, Al-Furuquni.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Victolina Ludovick akisoma hutuba katika maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akihutubia. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Mlulu.
 Wanafunzi wakipima urefu na uzito.
 Mtaalamu wa macho kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, Onesmo Magile, akimpima macho mtoto Spriani Issaya. Kushoto ni mama wa mtoto huyo, Elinaja Lissu.
 Mtaalamu wa macho kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, Julieth Tesha, akimuongoza kusoma herufi mgonjwa wa macho (hayupo pichani)
 Viongozi wa mkoa huo wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Dkt. George Mwakahesya cha kushiriki mafunzo ya upimaji wa viashiria vya awali vya saratani ya kizazi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahi na wanafunzi walokuwa wakimpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa.