Mkali mwingine wa Bongo Fleva kutoka kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, amemsihi bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba, aoe sasa kwani muda umekwenda na sherehe za watoto zimekuwa nyingi.



Rayvanny alimpa kubwa Diamond au Mondi katikati ya wiki hii, wakati wa arobaini ya mtoto wa jamaa huyo aliyezaa na mwandani wake wa sasa, Tanasha Donna, Naseeb JR iliyofanyika nyumbani kwa mama Mondi, Madale-Tegeta, nje kidogo ya Jiji la Dar.



“Kila siku bosi tunakuja hapa kwa ajili ya sherehe za watoto tu, tumechoka sasa, ifike mahali uoe sasa,” alisema Rayvanny huku Mondi yeye akiishia kumshangaa.

Kwa upande wake Mondi, alimwambia Rayvanny au Vanny kuwa kati yake na yeye ni nani wa kumshauri mwingine?



Mondi alisema maneno hayo kutokana na skendo ya hivi karibuni kuwa Rayvanny alizinguana na mkewe Fahyma aliyezaa naye mtoto mmoja, kiasi cha kudaiwa kuwa wameachana.



Kabla ya shughuli hiyo ya Naseeb JR, Mondi ameshaangusha pati za aina hiyo kwa wanaye watatu, Tiffah Dangote, Prince Nillan (hawa amezaa na Zari) na Dyllan aliyezaa na Hamisa Mobeto.