Mtayarishaji wa muziki nchini Kenya, Magix Enga amesema kuwa hatovumilia kuona wasanii wanatumia kazi zake (sampling) bila kibali chake na badala yake atawachukulia hatua kali.


Magix Enga na Harmonize
Akizungumzia suala la kuripoti YouTube wimbo wa UNO, Magix amesema kuwa alimpa wiki moja Harmonize kumuomba msamaha kwa kutumia vionjo vya kazi yake, Lakini hakufanya hivyo.

“Wiki moja imeisha na tayari wimbo wa Harmonize haupo tena kwenye mtandao wa YouTube. Nawaonya msijaribu kutumia midundo ya kazi zangu. Hii haitatokea tu nje ya nchi bali hata ndani ya Kenya.” ameeleza Magix Enga.

Producer Magix amelalamikia beat la wimbo wa UNO kufanana na beat la ngoma ya Dundaing.