MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amesema, kama waigizaji wa Bongo Muvi wangemjua Mungu, basi hata filamu zao zisingepoteza mvuto au tasnia hiyo isingekufa.

Pretty ambaye ameokoka na sasa anaimba nyimbo za Injili, ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, anatamani kila msanii amjue Mungu ili kwa nguvu zake, tasnia hiyo ifike mbali.

“Natamani kila msanii amjue Mungu kwani wote tungemjua Mungu, basi Bongo Muvi isingedorora au hata kusemekana imekufa kwani naamini kabisa kuna vitu vingi havimpendezi Mungu,” alisema Pretty.