HISTORI YA PICHA HIYO: 

Hii ndiyo ilikuwa picha ya mwisho kabisa ya Mwalimu Julius Nyerere kupigwa na mpigapicha wa Tanzania, Emmanuel Herman.

Ilikuwa saa nne asubuhi ya Jumanne 31 Agosti 1999 Uwanja wa Ndege Dar es Salaam, ambapo Mwalimu alikuwa akisafiri kwenda London kwa matibabu.

Maofisa usalama na walinzi walizuia waandishi kumpiga picha, ikawa tafrani baina ya waandishi na maofisa hao, lakini kwa umakini mpigapicha Emmanuel Herman, akapenya uzio wa Uwanja wa Ndege na kupata picha hii.

NB: Kwa taaluma ya habari, alichofanya Herman siku hiyo ni kitu kikubwa sana. Aliipa heshima kubwa taaluma yake na picha hii itabaki kama moja ya kazi kubwa alizowahi kufanya katika tasinia ya habari nchini.