Staa na Muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael "Lulu",  ameonekana kupagawa na kuweka hisia zake wazi juu ya wimbo wa Ali Kiba uitwao 'Mshumaa' baada ya kuona vijana wa kundi la Kings Music wakiimba wimbo huo kwa kutumia gitaa.



Lulu amepost video fupi katika mtandao wa kijamii wa Twitter ikiwaonyesha wasanii wa Kings Music, ambao ni Official Cheed na Tommy Flavour wakiimba wimbo huo live kwa kutumia gitaa kisha akaandika

"Niko mahali kwenye ukuta wa chupingi najikuna vipele vya baridi Goosebumps" ameandika Lulu

Staa mwingine aliyenogewa na wimbo huo ni Wema Sepetu ambapo kupitia mtandao wa Instagram alionekana akiongea na Ali Kiba kupitia video call ya mtandao wa Whatsapp kisha akaandika "Na mniache, Asante kwa hii track" .

Aidha kupitia ukurasa wa Instagram wa muigizaji Esha Buheti yeye aliandika kuwa "Weee  Ali sikuachii mpaka kufa"