Msanii kutokea visiwani Zanzibar, Nedy Music, amesema kuwa yeye ni mwanaume mpole aliyebakia duniani ila  anaogopa sana chozi la mwanamke kwa sababu anajua ni kitu kibaya kwa mwanaume.

Nedy Music ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akijigamba kuwa ni mwanume mpole asiyeumiza.

"Ni binadamu mpole pekee aliyebaki duniani kwa sababu katika vitu ambavyo nimewahi kuvifanya, naogopa chozi la mwanamke kabisa, najua ni kitu kibaya kwa mwanaume", amesema.

"Naogopa kumuumiza mwanamke na  kumfanyia chochote ambacho nahisi ataumia. Kuna muda unaweza ukawa umekosewa lakini ukaomba msamaha kwa sababu hutaki kumuona mtu huyo akiwa mnyonge au kujiskia vibaya pia", ameongeza Nedy.

Pia amesema kuwa yeye ni mtu mwenye imani ambapo anaamini katika kitu ambacho anajifunza kutokea kwa wazazi au kutokea kwenye dini, kwa hiyo vile ambavyo sio vizuri haitakiwi kuvifanya kwa mtu na hakutakiwi mwanamke alie kwa kosa ambalo sio.