MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni Video Vixen, Irene Louis ‘Lyyn’ amesema kuwa siyo kwamba anaringa kama watu wanavyomchukulia bali anajua kutafuta pesa ambazo ndizo zinazowafanya watu wengi wamuone kama anaringa. Lyyn aliiambia Mikito Nusunusu kuwa hela anazozipata kutokana na ishu zake tofauti, ndiyo anazitumia kujiweka kwenye maisha ya tofauti ili kukwepana na vitu mbalimbali kwenye jamii.

“Ninapoamua kuwa kivyanguvyangu watu wanadhani naringa kumbe najitahidi sana kutafuta hela ili niweze kuishi maisha yangu ninayoyataka na hii imeniepushia vitu vingi sana,” alisema Lyyn.